Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Z Anto amedai hawezi kuyakumbuka masuala ya kimapenzi aliyokuwa akiyapata kwa mpenzi wake wa zamani Sandra Khan maarufu kama 'Binti Kiziwi' kabla ya kufungwa jela huko nchini China kwa tuhuma za kubeba dawa za kulevya nchini humo.
Z Anto amebainisha kutokana kutomuona kwa kipindi kirefu mpenzi wake huyo anayetumikia adhabu ya kifungo chake na kusema anatamani sana arudi kitaa aendeleze maisha yake kawaida.
"Nafahamu kwamba yupo jela ila sifahamu anaendeleaje kwa wakati huu na pengine lini anatoka kwa sababu nimepoteza mawasiliano baadhi ya ndugu zake kwa hiyo sifahamu nini kinaendelea lakini mimi ni miongoni mwa watu wanaomuombea dua kama anaweza kutoka basi Mwenyezi Mungu amjalie atoke salama pia, kwa sababu hata kama tulikuwa na hitilafu sisi ni binadamu lazima tuombeane heri sina chuki naye", amesema Z Anto
Pamoja na hayo, Z Anto amesema miongoni mwa vitu ambavyo anavi-miss kutoka kwa 'Binti Kiziwi' ni pamoja na uwepo wake.
"Pengine angekuwepo wakati huu angekuwa amepiga hatua kubwa kimaisha kwa sababu marafiki zake ninao wafahamu wengi wapo vizuri sasa hivi. Nahisi kama angekuwepo angekuwa na 'channel' nyingi za kibiashara kwa wakati huu kutokana na jina alishakuwa nalo ila 'issue' za mapenzi na vitu vingine hapana siwezi kuvi-miss", alisisitiza.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top