Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii Timbulo ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Mshumaa' amefunguka na kusema hajui anapenda mwanamke wa aina gani kwani kila aina ya mwanamke huwa anamchanganya akili yake.
Timbulo anasema katika kipindi tofauti amejikuta akishindwa kujua aina ya mwanamke ambaye anastahili kuwa naye, kwani anaweza kukutana na mwanamke mnene akampenda, akakutana na mwanamke mwembamba akampenda, kuna muda anasema anapenda mwanamke mwenye rangi nyeupe lakini akikutana na mwanamke mweusi anachanganyikiwa. 
"Mimi mwanamke yoyote nampenda kuna wakati nilikuwa najidanganya kuwa labda napenda mwanamke mweusi lakini nikimuona mwanamke mweupe nawaka kweli, nikawa najiuliza hii inakuaje haya nasema napenda mwanamke vimodo lakini nikiona mwanamke mwenye umbo kubwa nachanganyikiwa, baadaye nikaja kugundua mimi mjinga moyo wangu unanidanganya, kumbe natakiwa kupenda kile ambacho kitakuwepo kwa wakati uliopo kwa hiyo mimi sijawahi kuwa na 'choice' kwamba napenda mwanamke wa hivi au hivi inategema na wakati tu siku zingine napenda mweusi, mweupe, mwembamba au unene" alisema Timbulo 
Mbali na hilo Timbulo alisema nyimbo zake nyingi huwa zinabeba ujumbe wa vitu vinavyo muhusu, hivyo kuna uhalisia mkubwa katika nyimbo zake na maisha yake ya kila siku.
Toka mwaka huu 2017 umeanza Timbulo ameshaachia ngoma nne ambazo ni Usisahau, Mfuasi, Ndotoni pamoja na wimbo huu mpya Mshumaa.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top