Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya kuchuniana kwa kipindi kirefu, hatamaye msanii wa RnB Bongo, Rama Dee amemaliza tofauti yake na kituo cha radio cha Clouds Fm.
Kupitia kipindi cha XXL Rama Dee alitumia fursa hiyo kuomba radhi kwa yote yaliyotokea kipindi cha nyuma na kueleza kuwa ni muda wa kufanya muziki mzuri.
“Mimi nasema kwa mashabiki wangu wote wa Clouds Fm na kote wanakonisikiliza, sasa hivi ni muda wa sisi kukaa sehemu moja. Kwa hiyo, kwa chochote ambacho kimetokea kwa Rama Dee ambacho kilionekana si sahihi, naweza kusema I m sorry” amesema Rama Dee na kuongeza.
“Na kwa Clouds Fm kwa wao wenyewe wanaona kwamba kuna sehemu walinikosea, tayari tumeshazungumza na tumeshamaliza kwa hiyo tupo sehemu nzuri na bila shaka upendo uendelee,” alimaliza kwa kusema.
Ikumbukwe kuwa Rama Dee ndiye aliyekuwa akifanya chorus katika ngoma za ‘kundi’ la Anti-Virus ambalo lilitoa albamu za kukishambulia kwa maneno kituo hicho cha radio, hata hivyo Rama Dee amesema katika albamu zilizotoka hakuna sehemu aliyotukana.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top