Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa Bongo Flava, Linex ametoa kauli ambayo haijaeleweka mara moja iwapo imemlenga rapper Nay wa Mitego.
Muimbaji huyo alipoulizwa ni kwanini sasa hivi hakuna hit song kubwa ingawa wasanii kila siku wanatoa nyimbo, alijibu kwa sasa kuna vitu vingi vinavyowateka watu nje ya muziki.
“Matatizo ni mengi, kwa mfano miluzi imekuwa mingi kuna vitu vingi vya kufuatilia apart from music, msema ovyo alipatia aliposema siasa inafunika muziki, unajua eeh?. Ni msema ovyo mimi namuitaga, sasa unaona yuko sawa yule?,” alihoji na kuendelea.
“Yule ni mshikaji wangu ila najua ni msema ovyo, hajawahi kunisema wala nini ila kuna vitu anaongeaga unaona kama huyu mtoto anadata,” Linex ameiambia Twenzetu ya Times Fm.
Katika wimbo wa Nay wa Mitego ‘Wapo’, kuna mistari inasema, “siamini nchi inaendeshwa kwa kiki, siasa inafunika muziki, viongozi wanashindana kukiki, wanagombea front page wauze kwenye gazeti”.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top