Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva nchini KR Mullah amesema msanii mwenzake wa bongo fleva Linah Sanga anamvuruga akili yake na kudai anatamani kumuoa binti huyo.
KR Mullah aliamua kujilipua na kuweka wazi hisia zake za mapenzi kwa mwimbaji huyo kupitia eNewz ya EATV na kusema anaamini ipo siku yeye ndiye atakuja kumuoa binti huyo kwa kuwa anampenda kupita maelezo.
"Dah yule mtoto yule nanvyompenda mwanangu hatari, yaani nitazidi kumpenda mpaka kesho kutwa, nasema lazima nitakuja kumuoa aiseee, namkubali sana na nampenda sana Linah".Alisisitiza KR Mullah 
Mbali na hilo KR Mullah ameamua kuweka tofauti zao pembeni na msanii mwenzake Juma Kassim Nature kama ilivyokuwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita ambapo KR Mullah alikuwa karibu sana na TID, KR Mullah anadai kuwa Temeke ndiyo nyumbani na Juma Nature ni mdogo wake hivyo ameamua kuonyesha upendo ikiwa pamoja na kupanda naye kwenye steji moja Jumamosi iliyopita kwenye show ya 'Heshima ya bongo fleva'


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top