Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ 
MSANII wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ juzikati alidaiwa kuzua timbwili la aina yake kwenye Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar baada ya tatizo alilolipata siku chache zilizopita la kudata kiakili kudaiwa kujirudia.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo hotelini hapo, mwanadada huyo alienda Lamada kumfuata msanii mwenzake Esha Buheti ambaye ndiye shosti wake mkubwa kwa sasa lakini alipoambiwa hayupo, ndipo alipowaanzishia timbwili wahudumu.
“Alizua timbwili la aina yake, ikabidi watu waliokuwa eneo la tukio wafanye kazi ya ziada kumtuliza.

“Baadaye ikabidi wamdanganye kwamba Esha yupo Muhimbili kapelekwa kujifungua, ndipo akacharuka tena akitaka apelekwe hukohuko akamuone, hawakumpeleka ila waliamua kumpakiza kwenye gari na kumzungusha maeneo mbalimbali ya jiji ili awe sawa,” alidai sosi huyo. Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kuona ana nafuu kidogo waliamua kumpeleka Mbagala ambako ndiko ndugu zake waliko.
Mr. Chuz

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, paparazi wetu alimvutia waya mtu wa karibu na Kabula ambaye ni mzazi mwenziye, Tuesday Kihangala `Mr. Chuz’ ambaye alieleza kuwa, amepewa taarifa na ndugu wa mwanadada huyo kwamba bado hayupo sawa kiakili na anatafakari jinsi ya kumsaidia ili aweze kupona kabisa. “Leo (juzi) hii ndugu zake wamenitaarifu kwamba bado hajawa sawa na hali yake inawachanganya sana, walinipa niongee naye ili niamini, yaani anaongea maneno mengi mfululizo, kwa kweli anahitaji matibabu ya kina kabla ugonjwa haujakolea,” alisema Chuz.

Jini Kabula hivi karibuni alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akidaiwa kuchanganyikiwa akili lakini siku chache baadaye alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kabla ya juzi mambo kudaiwa kuharibika tena.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top