Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa muziki wa bongo fleva Enock Bella ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi la Yamoto Band amefunguka na kusema muda wake kwenye muziki bado huku akidai saizi muziki unaushindani ambao hawezi kushindana nao akiwa mwenyewe. 
Enock Bella alisema hayo alipokuwa akihojiwa na eNewz na kusema kuna moja ya wimbo wake umevuja lakini yeye hawezi kuupa nguvu kwa kuwa hakuuachia yeye wimbo huo na kusema muziki wa sasa unahitaji mtu uwe umejipanga kwani ukifanya mchezo unaweza kupotea kabisaa kwenye ramani. 
"Kuna wimbo ulivuja lakini kwa kuwa mimi sikuutoa ilikuwa ni vigumu mimi kusimama nyuma ya wimbo huo na kuupa nguvu, mimi muda wangu wa kuachia wimbo na kutoka mwenyewe bado saizi angalia mwenyewe muziki jinsi ulivyokuwa na ushindani mkubwa, ukifanya kazi ili mradi iende utakuja kupotea mapema. japo saizi nipo na menejimenti lkini nategemea kupata uongozi uliomadhubuti ambayo nikikaa nayo nikianza kutoa kazi ni mpera mpera na si kurudi nyuma"alisema Enock Bella 
Mbali na hilo Enock Bella anasema management ambayo yupo nayo sasa bado hajasaini nayo mkataba wowote ule ila anafanya tathimini kuona jinsi gani hao watu wanaweza kufanya naye kazi, na jinsi gani anaweza kunufaika na uongozi huo.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top