Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Wakati mashabiki wa Bongo Fleva wakisubiria video ya kundi la Weusi ‘Amsha Dude’, kuna uwezekano mchekeshaji aliyejizolea umaarufu mkubwa katika mitandao hivi karibuni, Ebitoke akatokelezea katika video hiyo.

Rapper wa kundi hilo, Joh Makini amesema kwa sasa wanawaangalia wale ambao wamekuwa wakiwatumia clip za video kuhusu ngoma yao ya Amsha Dude ili waje kuwatumia katika official video ila kwa wale waliofanya vizuri zaidi.
“Katika hizi baadhi ya clap watu wanatuma tumependezwa na baadhi ya watu wanavyofanya, kuna comedian kama wakina Ebitoke, kuna dogo anaitwa Whozu  na wengine sijawataja majina pengine yamenitoka kidogo wale tutawatumia kwenye video, tutaongea nao,” Joh Makini ameiambia Daladala Beat ya Magic FM na kuongeza.
“Kwa hiyo kama wenyewe wanasikia sisi tunawashukuru kwa njia moja ama nyingine waendelee kuupa wimbo wetu mirage. Watengemee shavu na yeyote ambaye anaweza akafanya au ana crazy dance ya Dude ambayo haijapigwa, tukiikubali anapita kwenye usahili kwa sababu hii ni ya watu,” amesisitiza Joh Makini.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top