Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa bongo fleva Chin Beez amefunguka na kumjibu rapa Chid Benz kuhusu jina lake na kusema yeye haoni sababu ya kubadili jina hilo kwa kuwa haoni kama linafanana na jina la Chid Benz.
Chin Beez alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kudai siku zote hajawahi kusikia mashabiki wakisema majina hayo yanafanana hivyo haoni sababu ya kubadili jina lake licha ya rapa Chid Benz kumtaka kubadili jina kwa madai ya kuwa linafafa na jina lake.
"Mimi siwezi kubadili jina sababu jina langu halifanani na jina lake, kwa hiyo kuna utofauti mkubwa kati ya jina langu na lake. Mimi nafanya vitu vyangu na kufanya muziki wangu siwezi kukaa saizi napigania jina saizi mimi napigania muziki wangu, 'Chin' kila mtu anajua maana yake ni kidevu kwa hiyo ndiyo maana nilijiita Chin Beez  kwa sababu hiyo" alisisitiza Chin Beez 
Kupitia Planet Bongo rapa Chid Benz alimtaka Cheen Beez kubadili jina lake na kusema kuwa msanii huyo ameiga jina lake hilo hivyo anapaswa kubadilisha na kutafuta jina jingine ambalo halitafanana na Chid Benz.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top