Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa Bongo Flava, Chege ametaja ngoma zake mbili alizitoa miaka ya hivi karibuni ambazo hazikufanya vizuri.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Go Down ametaja nyimbo hizo kuwa ni Chapa Nyingine na Kelele za Chura ambazo hazikufikia kiwango alichokuwa akikitaka.
“Kuna ngoma kama Chapa Nyingine haikufanya vizuri, Kelele za Chura haikufanya vizuri ingawa ina viewers zaidi ya milioni moja lakini haikufika vile nilivyokuwa nataka,” ameiambia 5 Selekt ya EATV na kuongeza.
“Mimi nafikiri kukubali matokeo ndio unaweza kutengeneza ngoma nyingine nzuri, hata unavyoniona nipo sio kwamba ngoma zote zinafanya vizuri, kuna ngoma mbazo huwa zina bounce zinapotea, tunatoa nyingine sinakuja ku-save zile zilizopita,” amesisituiza.
Chege kwa sasa anafanya vizuri na ngoma mpya ‘Najiuliza’ ambayo amewashirikisha Ray C na Sanaipei Tande.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top