Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Sabrina Omary ‘Sabby Angel’

SIKU chache baada ya kutangaza kuachana na sanaa, mrembo aliyekuwa akifanya filamu na muziki wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amesema kuwa, anajuta kuwa msanii kwani maisha yake yameharibika kwa kiasi kikubwa.

Akipiga stori na Star Mix, Sabby aliyewahi kubamba na Wimbo wa Inahusu na Tamthilia ya Talaka amesema sanaa imemuharibia CV yake kwenye jamii, pia amekuwa akiendelea kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakimuomba penzi.

“Jinsi nilivyo na maisha ninayoishi ni tofauti kabisa na kazi hiyo niliyokuwa naifanya, siwezi tena kamwe kuwa msanii, nilivyosema nimeacha watu walidhani natania wakidhani ipo siku nitarejea kwenye fani, hakika sanaa imeharibu maisha yangu, kwanza usumbufu ulikuwa mkubwa, kila mtu ananitaka hadi kero,” alisema.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top