Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa Bongo Flava ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Wasikudanganye’, Nandy ametaja sababu ya mkali wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol kuwepo katika video ya wimbo huo.
Hitmaker huyo wa wimbo ‘One Day’, ameiambia FNL ya EATV kuwa yeye pamoja na team yake ambayo wanashirikiana katika kazi waliona Ben Pol anafaa kuwepo katika nafasi hiyo.
“Kwa sababu nilikuwa nataka nimuweke msanii mwenzangu na katika wasanii tumeona msanii ambaye mimi naweza kuendana nae ni Ben Pol. Mimi na Ben Pol tunaendana, kwa hiyo tukaweza kufanya video ana anafiti ila character, kuna nakubaliabna ambayo tunayo,” amesema Nandy.
Ben Pol ambaye kwa sasa ameviteka vichwa vya habari kwa namna anavyo-handle couple yake yao na mchekeshaji Ebitoke, hivi karibuni pia alitokea katika video ya Jux ‘Umenikamata’ lakini katika angel tofauti.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top