Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya ku-'hit' na ngoma moja, msanii na mrembo Amber Lulu amedai hawezi tena kufanya kazi ya kupendezesha nyimbo za wasanii kwani kufanya hivyo ni kumrudisha nyuma badala ya kusonga mbele.
“Sasa hivi nafanya muziki sio video vixen tena kwa sababu nimeshaingia kwenye muziki kwa hiyo nikifanya video vixen nakua kama narudi nyuma na mimi sitaki kurudi nyuma tena nahitaji nifanye vitu vipya. Inatakiwa kama ni muziki wangu niufanye wa international au nizidishe sitaki kurudishana nyuma" alifunguka kwenye eNewz.
Hata hivyo amber amesema amekuwa akipokea maoni tofauti tofauti kutokana na wimbo wa 'Watakoma' wengi wakitoa sifa na kumtia moyo.
"Napokea maoni mengi mazuri, mfano kuna baadhi ya wasanii kama wakina Shilole na Chege nimeshakaa nao kuna vitu wameniambia unatakiwa ufanye,” aliongeza.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top