Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosa amevikana vichwa vya treni ambavyo vipo bandarini na kusema katika kipindi chote wakati yeye anatumikia nafasi hiyo hajawahi kusaini mkataba wowote wa kuingiza vichwa hivyo nchini.
Masanja Kadogosa amesema kuwa TRL wao hawajahusika kufanya biashara hiyo na kampuni yoyote ile na kudai uchunguzi ndiyo unaweza kuleta majibu vichwa hivyo ni mali ya nani kama ambavyo Mhe. Rais John Pombe Magufuli alivyoagiza 
"Unapozungumzia tumeagiza vichwa vya treni ni kwamba lazima kuwe na muuzaji na mnunuaji na kuna huduma za malipo, TRL haijafanya 'transaction' wala hatujaingia mkataba wowote na mtu yoyote kutuletea vichwa vya treni nchini, mambo mengine yatafahamika baada ya kufanyika kwa uchunguzi kwani ndiyo  litakuja kuwa wazi kwamba nini kimetokea, lakini kama tulivyosema TRL pamoja na mimi kwa mwaka wangu mmoja niliokaa hapa sijasaini mkataba wowote na mtu yoyote kwa ajili ya kuletewa vichwa hivyo ambavyo vipo bandari. Tumeshawambia hata bandari kuwa vichwa hivyo hatujaviagiza sisi, hatujawaambia kutuletea na hatujatuma mtu yoyote kukamilisha malipo sababu si vyetu" alisema Masanja Kadogosa Mkurugenzi wa TRL 
Siku ya Jumapili ya tarehe 2, Juni 2017 Rais Magufuli alikwenda kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa bandari ambapo aligundua kuna zaidi ya vichwa 10 vya treni ambavyo havijulikani ni mali ya nani, wala haijulikana vimeagizwa na nani, hivyo aliagiza uchunguzi ufanyike na ifahamike vichwa hivyo vya treni vimeletwa na nani nchini. 


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top