Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mwanamume mmoja raia wa Ufaransa ameshtakiwa kupanga njama ya kuuawa kwa rais Emmanuel Macron katika makumbusho ya Bastille kwenye gwaride la kijeshi.Siku hiyo ya makumbusho hufanyika kila Julai 14 na mwaka huu rais Macron alimwalika rais Donald Trump.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 23 aliambia polisi kwamba alikuwa amepanga pia kumuua rais Macron Julai 14 ambapo ilikuwa siku ya gwaride la taifa jijini Paris .
Aliendelea kufahamisha kwamba alikuwa na mipango ya kushambulia waislamu,Mayahudi ,watu weusi na pia wapenzi wa jinsia moja .Polisi walimkamata mtu huyo Jumatano iliyopita katika mitaa ya kaskazini magharibi ya jiji la Paris .Macron alimkaribisha rais Donald Trump kama mgeni maalum katika makumbusho ya Bastille ya uvamizi wa gereza mnamo mwaka 1789 .


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top