Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya kuwepo kwa taarifa za kutoweka ghafla kwa Meneja wa kitengo cha ICT ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya IEBC, Chris Musando, leo July 31, 2017 imeripotiwa amekutwa akiwa amefariki.
Imeelezwa kuwa mwili wa Chris Musando aliyekuwa Meneja wa masuala ya Teknolojia wa IEBC, umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi huku mawasiliano yake ya mwisho yakiwa kwa njia ya SMS na mmoja wa wafanyakazi mwenzake siku ya Jumamosi majira ya saa tisa usiku.
Tukio hili linatokea ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Kenya ambao utafanyika tarehe 8 August.
Polisi wanasema kuwa miili ya Afisa huyo pamoja na mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo vitongoji vya mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top