Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Prodyuza Maxmaizer amempa sifa kibao msanii wa Bongo Flava, Beka Flavour kuhusiana na uwezo wake mkubwa wa kazi.
Maxmaizer ambaye ndiye ametengeneza hit song ‘Libebe’ ya msanii huyo, ameiambia Safari Radio kuwa Beka ni msanii mzuri anapokuwa studio na anapoelekezwa anaelewa mara moja.
“Beka ni msanii ambaye mkienda kurekodi ananyoosha, ni msanii mzuri kwa sababu ana vocal nzuri na pia kabla ya kurekodi wimbo anapitia kwenye academic anakaa na kujifuza kuimba, so akija studio ananyoosha moja kwa moja, sijapata shida sana katika uingizaji wa vocal, ni mara moja tu anaingiza,” amesema Maxmaizer.
Kuhusu ugumu alioupata katika kurekodi ngoma hiyo, Maxmaizer amesema, “ugumu upo kwa sababu nilikuwa natafuta kutengeneza wimbo mzuri, kuhakisha beat inakuwa nzuri na yeye anaimba vizuri na ninafanya mixing nzuri,” amesistiza.
Ukiachilia mbali hit ya Beka ‘Libebe’, Maxmaizer ametengeneza hits kama Iyola ya Harmonize, Sielewi ya Chemical na Mfuasi ya Timbulo.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top