Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail ThisWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa nne kushoto) akiwa na familia yake wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu mkewe, Linah George Mwakyembe katika Kanisa la KKKT Kunduchi jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Jenister Mhagama (wa pili kushoto)akiaga mwili wa marehemu Linah Mwakyembe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mwili wa marehemu.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Saleh Ally akipita kuaga mwili wa marehemu.

Wasanii Dokii na Single Mtambalike ‘Richie’ wakiaga mwili wa marehemu.

Waombolezaji wakiaga.

Mdau wa Michezo, Abbas Tarimba akiaga.

Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo akiaga.

Aliyekuwa Kocha wa Klabu ya Mwadui, Jamhuri Kihwelo akiaga.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Samia Suluhu Hassan amewaongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bi. Linah George Mwakyembe  katika Kanisa la KKKT lililopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

Wakati wa kuaga mwili wa marehemu Linah, viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Katibu Mkuu balozi John Kijazi na wengine walipata fursa ya kutoa salam za pole kwa familia ya Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na ndugu yao kipenzi.

“Tunajua Linah alikuwa zaidi ya kila kitu kwenu, lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kazi yake. Alimleta dada Linah duniani, alitupa amana yake na leo ameinyakua. Sisi tulimpenda lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!” alisema Samia.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top