Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Italia. Mkurugenzi mpya wa michezo wa klabu ya AS Roma, ameitahadharisha Manchester United isipoteze muda wake kuhusu mpango wake wa kumsajili mchezaji wao, Radja Nainggolan kwani haendi popote katika msimu huu wa kiangazi.Raia huyo wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kujiunga na Mashetani Wekundu, pia mwaka jana klabu ya Chelsea ilikaribia kumsajili lakini mpango huo ukayeyuka.
Mchezaji huyo mwenye miaka 29 ameimarika kuwa miongoni mwa viungo tishio duniani, hivyo uongozi wa klabu hiyo ya Italia imetangaza rasmi haitamuachia kwenda klabu yoyote msimu huu wa kiangazi.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top