Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mkali wa muziki wa singeli Bongo, Man Fongo amekubali yaishe baada ya kumaliza tofauti zilizokuwepo kati yake na meneja wake wa zamani, kutoka 'Makers Entertainment' G Maker kwa kurudi na kuomba radhi.Msanii huyo aliyetamba na ngoma ya ‘Hainaga ushemeji’ mwaka 2015 akiwa chini ya usimamizi wa G Maker, aliingia katika ‘bifu’ kali na meneja wake huyo katikati ya mwaka 2016- 2017 huku chanzo kikitajwa kuwa ni kutofautiana katika suala la pesa.
Baada ya kutengana kwa takriban mwaka mmoja, Man Fongo ambaye ametambulisha rasmi ngoma yake mpya jana aliyoipa jina ‘popcorn’, amesema aligundua kosa lake na kuamua kurudi kwa G Maker, kwa kuwa aliona hawezi kuwa mbali naye kikazi kutokana na uhusiano wao kama ndugu.
“G Maker mimi ni kama kaka yangu….. Mimi ndio nilimfuata, nilikwenda kwake na kuomba tuyamalize yale matatizo hivyo saizi nimerudi kwenye uongozi wangu wa zamani,” Man Fongo amefunguka kwenye East Africa radio.Ngoma ya Man Fongo aliyoiachia jana ipo chini ya uongozi wa G Maker na huku mpikaji wa ngoma akiwa ni Mensen Selekta ambaye kwa pamoja hiyo ndiyo timu iliyotengeza 'hit' ya 'Hainaga Ushemeji'.
Msanii huyo amesema video ya ngoma hiyo ipo katika hatua za mwisho, na wakati wowote itakuwa hewani.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top