Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msichana mmoja kutoka Kenya aliyefahamika kwa jina la Nuru Hatim akiwa na mtoto anayedaiwa wa Ali Kiba.
SKENDO ‘hot’ inayomhusu staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ ya kudaiwa kuzaa na msichana mmoja kutoka Kenya aliyefahamika kwa jina la Nuru Hatim kisha kumtimua, imechukua sura mpya baada ya mama wa msanii huyo kuzungumza na gazeti hili na kutema cheche, Ijumaa linakujuza.
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’.
KUHUSU BINTI MKENYA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Nuru alitua Bongo akitokea nchini Kenya na kwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Msimbazi na pia Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania kwa ajili ya kuomba msaada wa kumpata Kiba sambamba na kuomba msaada wa kisheria akidai amezaa na staa huyo kisha kuachwa kwenye mataa.
Staa wa Bongo, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’.
TUJIKUMBUSHE KWANZA ALICHOKISEMA NURU
“Mwaka jana nikiwa Mombasa, Kiba ambaye tulikuwa tukijuana na kuwasiliana kwa muda mrefu, alikuja kufanya shoo na ndipo tulipofanya tendo la ndoa.
“Mara kadhaa tulikuwa tukikutana kwa kutumia kinga lakini safari hiyo, hatukutumia na ndipo nikanasa mimba.
“Baada ya kunasa mimba, familia ilinijia juu na kutaka kujua mhusika, nikawaambia ni Kiba ndipo nilipofukuzwa na kwenda kuishi na rafiki zangu. Kiba alikuwa hapatikani mpaka najifungua, ndiyo nikaja Bongo na kwenda nyumbani kwa akina Kiba ambapo mama yake aliniambia hayupo, amesafiri,” alisema msichana huyo aliyekuwa amempakata mtoto anayeonekana kufanana na Kiba.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top