Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas `Lulu Diva’.
MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas `Lulu Diva’ amejikuta kwenye furaha ya aina yake baada ya kuingia mkataba na msanii kutoka nchini Kenya,Jaguar atakayekuwa anasimamia kazi zake.
Akipiga stori na Showbiz Xtra,Lulu alisema ni jambo la kujivunia kupata shavu kama hilo kwani hakutegemea kama angeweza kupiga hatua kimuziki na kazi zake kusimamiwa na mtu kama huyo mwenye heshima kubwa kwenye gemu ya muziki.“Namshukuru Mungu kwa hili, nimepata mkataba mnono kwa Jaguar, makazi yangu yataendelea kuwa Bongo, lakini inapotokea nikahitajika Kenya nitakuwa nafika kwa wakati, niwaombe mashabiki wangu waendelee kunisapoti, naamini nitafika mbali zaidi na kuiwakilisha vyema nchi yangu,” alisema huku akigoma kufafanua ni mkataba wa muda gani


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top