Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya tetesi za muda mrefu kuhusiana na club ya Arsenal kuhusishwa kumtaka mshambuliaji wa Olympique Lyon Alexandre Lacazette, jana July 4 mshambuliaji huyo alikamilisha mpango wa kufanya vipimo vya afya na leo amejiunga na Arsenal.
Arsenal imefanikiwa kumsajili Alexandre Lacazette kwa mkataba wa miaka mitano, Lacazette ambaye anaichezea pia timu ya taifa ya Ufaransa amedumu na club ya Olympique Lyon toka 2010 alipopandishwa kutoka timu B.
Lacazette ana umri wa miaka 26 na amejiunga na Arsenal kwa dau la usajili wa linalotajwa kufikia pound milioni 53, hadi anajiunga na Arsenal alikuwa kaichezea Lyon jumla ya mechi 203 za Ligue 1 katika misimu nane, akifunga magoli 100, msimu uliopita kafunga jumla ya magoli 28 katika mechi 30, ametengeneza nafasi 247 na kutoa assist 21 katima misimu yake nane.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top