Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Majeruhi Tabia Mbonde akiuguza majeraha aliyoyapata kutokana na kushambuliwa.

INATISHA sana! Hii ni simulizi ya mwanamke ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Rwaruke, Kibiti mkoani PwaniTabia Mbonde ambaye ameshuhudia mumewe, Ramadhani Mzuzuri akiuawa mbele yake kisha naye kumim­iniwa risasi tano
baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa miongoni mwa kundi linaloendeleza mauaji maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji, Risasi Jumamosi lina mkasa nzima.
Baada ya kutokea tukio hilo, mapema wiki hii, wa­nahabari wetu walifika ki­jijini hapo kisha kumfuata Tabia aliyelazwa kwenye Hospitali ya Mchukwi iliy­opo Songa, Kibiti ambaye alianika simulizi nzito ya jinsi walivyovamiwa hadi mumewe kuuawa na yeye kujeruhiwa kwa idadi hiyo ya risasi.
SIKIA SIMULIZI HII
Huku akiugulia mau­mivu makali akiwa wodini hospitalini hapo, Tabia al­isema kuwa, siku ya tukio, majira ya usiku, wakiwa wamepumzika, walishtu­kia wamevamiwa na watu wenye silaha waliokuwa wakimhitaji mumewe Ra­madhani.
“Walikuja na (Toyota) Noah nyeupe mpaka kar­ibu na nyumba yetu kisha wakavamia nyumba na kuvunja mlango.


Ramadhani Mzuzuri enzi za uhai wake.

“Baada ya kuvunja mlango, walikutana na mimi uso kwa uso. Nili­waona watu watatu ware­fu waliokuwa na silaha na hapo nikajua kabisa kuwa tulikuwa tumesha­vamiwa.
“Waliniuliza kama mume wangu alikuwepo, nikawaambia hayupo.

“Nilipowajibu hivyo walionekana kutoniamini na kwamba walikuwa na uhakika kuwa yupo hivyo walianza kunipiga ngumi na mateke.
“Walikuwa waki­niambia kuwa wa­taniua kwa kujitakia mwenyewe kwani wao hawakuwa na shida na mimi, lakini kwa kuwa nil­ionekana kutowapa ush­irikiano, walisema lazima waniue.
“Wakati hayo yote yakitokea mume wangu alikuwa chumbani na alikuwa anasikia tunavy­olumbana.
MUMEWE AJIFICHA DARINI
“Alichokifanya mume wangu kwa kujua kabisa kuwa watu hao hawata­muacha hai, alipanda darini kujificha akidhani angeinusuru roho yake lakini pamoja na jitihada zote hizo umauti ulimkuta (kilio cha kwikwi).
“Baada kuona wanazidi kunitesa pale mlangoni, niliwaponyoka na kuanza kuwakimbia lakini kabla sijafika mbali walinimim­inia risasi mfululizo zipa­tazo tano ambapo zilinije­ruhi miguu yote.


Tabia Mbonde akionyesha majeraha yake.

“Risasi nyingine ili­nipiga kutokea nyuma kwenye ubavu wa kulia na kunitoboa titi kama hivi mnavyoniona (akionesha jeraha la risasi kwenye titi).
“Walipoona hilo halito­shi, waliendelea kunikim­biza hadi kwenye kichaka kilicho karibu na nyumba yetu ambapo waliendelea kunipiga risasi nyingine.

“Baada ya kunipiga risasi nyingi na hasa ile waliyonipiga uba­vuni, waliona siwezi kupona tena hivyo wakaamini nimekufa na nilimsikia mmo­ja wao akiwaambia wenzake huyo tayari twendeni ndani tu­kamtafute mumewe,”alisimulia Tabia huku akieleza kuwa alikuwa akishuhudia kila kitu wakat i mumewe akiuawa kwani alikuwa akio­na na kusikia lakini hakuwa na uwezo wa kusimama au kupam­bana.

Afisa Tawala Hospitali ya Mchukwi, Yasinta Maneno.

RISASI ZARINDIMA KWA SAA 2
Tabia aliendelea kusimulia kwamba, tukio hilo lilichukua zaidi ya saa mbili huku risasi zikir­indima, lakini katika hali ya kustaajabisha hakukuwa na msaada wowote kwani wana­kijiji waliogopa.
“Wale wauaji, baa­da ya kuona wame­shanimaliza walimru­dia mume wangu na kuanza kumtafuta mle ndani. Kumbe alikuwa amejificha darini.
“Katika kutafuta niliwasikia wakisema kuwa wamemuona ndipo wakaanza kum­shambulia kwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Walianza kum­miminia risasi akiwa mlemle darini kabla ya kumshusha na kuen­delea kumpiga risasi. Mume wangu alikuwa akijitahidi kujiokoa la­kini ulifika muda aka­dondoka mlangoni na nikamshuhudia akikata roho.…Akizungumza na Global TV Online.


“Pamoja na kwamba nilikuwa na maumivu makali, la­kini siwezi kusahau ile picha ya mume wan­gu kukata roho. Inau­ma sana, nadhani kwa wanawake wenzangu wanajua maumivu ya zaidi ya uchungu.
“Huo ndiyo ukawa mwisho wa uhai wa mume wangu na hadi nipo hapa hospitalini sijui chanzo ni nini kwa sababu hatuja­wahi kupata hata vit­isho vya aina yoyote,” alisema Tabia, mama wa watoto wawili alio­zaa na mumewe huyo akiwemo wa miezi mi­tatu aliyekoswakoswa na risasi na kuongeza: “Namshukuru Mungu nimepata matibabu tangu nilipoletwa hapa usiku ule nikiwa katika hali mbaya na mume wangu ameshapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.”
SACP Onesmo Lyanga.

KAMANDA WA POLISI SASA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji (Mkiru), SACP Onesmo Lyanga alithibitisha kuto­kea kwa tukio hilo na kwamba oparesheni maalum ya kuwasaka wahalifu hao inaen­delea.
Mpaka sasa zaidi ya watu 35 wame­poteza maisha kwenye matukio ya mauaji katika wilaya hizo huku Jeshi la Polisi likiwa lime­jipanga vilivyo ku­komesha tatizo hilo.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top