Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya tetesi nyingi kuhusu ujio wa iPhone 8 wengi wakihoji muonekano wake utakuwaje na sifa nyingine tayari wataalamu wa teknolojia wameshavujisha muonekano wa simu hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na watumiaji wa simu hizo na inatarajiwa kutoka Septemba mwaka huu.
Video inayoonesha muonekano wa simu hiyo imevujishwa na mtandao wa stevehemmerstoffer.com  na inaonesha muonekano wa simu hiyo vizuri kabisa ambapo unakupa nafasi ya kuhakiki baadhi ya sifa ambazo awali zilikua ni tetesi tu kutoka kwenye mitandao mingine duniani.

Sifa nyingine itakuwa na Wireless Charger, Camera ya mbele na Home Button zitakuwa kwenye kioo (Display), Kamera ya nyuma itakuwa na Mega Pixel 12 na ya mbele Mega Pixel 8 na gharama yake itakuwa ni zaidi ya dola $1000 sawa na Tsh milioni 2.2 kutegemeana na ukubwa wa simu.
Je, mdau wa simu za kampuni hiyo pendwa kabisa duniani umeupokeaji ujio wa simu hii? na muonekano wake unauonaje?


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top