Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mastaa Hamad Ally Seneda ‘Madee’ na Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ wakiwa wameshikana mikono.
MAISHA yana sarakasi na madoido mengi kupindukia. Huyu akiibuka na janga hili, yule anachomoza na kioja kile ilimradi tu dunia inajizungusha kwenye mhimili wake na kutengeneza usiku na mchana.
Mastaa wana ‘vichaa’ vingi ambavyo ukivitazama kwa jicho la tatu, hakuna kingine cha kufanya zaidi ya kupigwa butwaa kisha kumrudishia muumbaji utukufu. Lipo lile suala la watu wengi maarufu ndani na nje ya Bongo, kutengeneza uhusiano wa kimapenzi ambao kimsingi hauna ukweli wala uhalisia wowote, kinachokuwa kimemaanishwa ni kile kinachoitwa ‘ku-make headlines na ku-draw attention’.
Mjumuisho wake ni kiki. Angelina Jollie, kabla ya kuungana kiukweliukweli na Brad Pit, walianza uhusiano wa kutafuta kiki ikiwa ni njia ya kuitangaza filamu waliyoigiza pamoja na Mr & Mrs Smith, lakini baadaye waliamua kuingia moja kwa moja na kujikuta wakizaa pamoja.
Uhusiano wa namna hiyo umezagaa kwa mastaa wengi, Kibongobongo hali imekithiri na kila kukicha ‘kapo’ nyingi zinazaliwa lakini mwendelezo wake huishia kusikojulikana na ukichunguza kwa umakini, unagundua kilichokuwa kinaandaliwa ama ni wimbo au filamu mpya.
Shilole akifanya yake.
Yupo mwanamuziki ambaye alitumia sana mgongo wa kapo zisizokuwa na mashiko kumfikisha juu. Hapa chini nitaainisha baadhi ya mastaa Bongo ambao walijaribu kutumia nafasi hii kwa kuwahadaa mashabiki wao kwa kiki za kimapenzi.
MADEE NA LULU DIVA
HII ndiyo imeshtua! Hivi karibuni gumzo kubwa limekuwa ni kapo ya Hamad Ally Seneda ‘Madee’ na Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambao wametengeneza ‘atensheni’ ya kufa mtu, baada ya kunaswa wakiwa pamoja kwenye moja ya kumbi maarufu za starehe, wakionesha kila lililopaswa kufanywa na wapenzi walioshibana kwa kiwango pitilizi, kwa sasa Madee na Lulu Diva wanatoka na kutembea sehemu mbalimbali za jiji kwa madaha ya kimapenzi, kifupi ni kwamba wametengeneza kapo, ambayo binafsi moyoni naisikia sauti ikiniambia kwa uzito wa besi kuwa, kuna kazi itafuata baada ya fujo zote hizo, ni kapo feki ya kutafutia mapokezi ya kazi, tusubiri
SHILOLE NA HAMADAI
NADHANI hadi leo watu wengi huamini kuwa wanatoka kimapenzi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu ana maisha yake na walitengeneza mazingira hayo ili kushika na kuteka hisia za wadau na wapenzi wa sanaa ya vichekesho na kweli walifanikiwa. Lakini mwisho wa siku ilibainika kuwa ukaribu na kapo yao ililenga hicho nilichoainisha hapo juu, kiki za kazi.
WAKATI Zuwena Mohamed au Shishi Baby kama akiwa njiani kuachia Ngoma ya Sitoi Kiki, habari iliyosumbua ngoma za masikio ni uhusiano wake na mwanamuziki mchanga, Hamadai. Penzi likawa penzi la kwelikweli, mara ikawa Shilole amempora mwanaume huyo kwa mwanamke, kapo yake ikadumu hadi wimbo ulipotoka, siku chache hakuna cha mapenzi, mahaba wala uhusiano, kiki iliisha na kazi yake ilimalizika.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top