Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’ na mama yake Halima Hassan.
  Mama mzazi wa Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’, Halima Hassan anadaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Ugandaakisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.
“Tangu Ivan afariki dunia afya ya mama Zari imekuwa ikizorota siku hadi siku kutokana na wawili hao kuwa na maelewano ya karibu na mazuri,” kilisema chanzo na kuongeza;
“Kwa sasa anapumua kwa kutumia mashine ya oksijeni. Wiki iliyopita Zari na dada zake walilazimika kurejea haraka nchini (Uganda) wakitokea Afrika Kusini baada ya kupata taarifa za kuzidiwa kwa mama yao.”
Hata hivyo, Jumatatu ya wiki hii ilitolewa taarifa kuwa Zari na madaktari wanaomuuguza mama yake walikuwa kwenye mazungumzo ya siri kutokana na afya ya mama yake kutoridhisha.
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, ni Zari na dada yake pekee ndiyo wanaoruhusiwa kumjulia hali mama yao na kama hali yake itakuwa hairidhishi basi watalazimika kumsafirisha.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top