Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Baada ya kuripotiwa story inayomuhusu aliyekuwa Stylish wa Diamond Platnumz, Qboy Msafi kudaiwa kumpa ujauzito msichana wa miaka 18 na kumtelekeza, mama mzazi wa msichana huyo ameahidi kulisimamia.

Soudy alipiga story na Qboy Msafi na Mama mzazi wa msichana huyo ambao kila mmoja alizungumza kwa upande wake huku Qboy akisisitiza kuwa ujauzito huo haumuhusu wakati mama wa msichana akisema anachokifanya Qboy sio kizuri na atafuata sheria kuhaikiksha binti yake anapata haki yake.
“Media ndiyo nani? Hizo drama, halafu Soudy si unajua mimi mwanao sina mambo ya kufuatilia drama. Hakuna mimba, hakuna kitu kama hicho. Kwanza yeye mwenyewe hanijui.  Soudy unaposikia habari, sikiliza upande wa pili, asije mtu akawa anakuhadithia kwa kukutengenezea picha zake. Mimi sina mapicha picha, nafanya issue zangu ambazo zinanitangaza.
“Hata hilo suala nilikuwa sijui. Nimeona watu wakinitag kwenye Instagram. Ndio maana sikutaka kuzungumzia lolote. Hapa nyuma media zilikuwa zinanizungumzia katika vitu vingi sana, so, issue kama hizo naona wananifungulia dunia.” – Qboy Msafi.
“Huyo ndiyo aliyempa ujauzito mpaka tarehe na kipindi amempa ujauzito akamsababishia mwanangu akagombana na mtu kwa sababu yake na kapata majeraha. Yote mimi nimenyamaza lakini yeye angekuwa mstaarabu angekubali tu amsaidie mwanangu kwa sababu tayari kasababisha amecha shule mpaka mimi nahangaika naye na miezi inakaribia kujifungua. Kamuharibu mwanangu halafu anakataa ina maana huyu mtoto mdogo hana akili aseme mimi nimefanya hivi na amsingizie fulani tu au kwa sababu ni msanii!
“Mimi ninachotaka ni bora anipe msaada kwa binti yangu sitaki tumtese huyu kiumbee. Kama atakataa nitafuata sheria ifuate mkondo wake maana ndio anachotaka. Ni mzazi gani atakayevumilia mpaka binti anafikisha miezi saba?” – Mama Media.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top