Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ameizungumzia ngoma yake mpya ‘Unanionaje’ aliyofanya na Harmonize.
Rapper huyo kutoka Rocky City Mwanza, ameiambia Clouds FM kuwa kutoa ngoma hiyo na Harmonize haimaanishi kuwa amejiunga na label ya WCB ila ni watu anaofanya nao kazi kwa ukaribu zaidi kwa kipindi hiki.
“Namshukuru sana Harmonize pamoja na uongozi wake wa Wasafi kwa kufanikisha kazi hii na kunipa ushirikiano mpaka video. Ngoma inaitwa Unaionaje lakini mwanzoni nilipenda iitwe Kunja lakini kiitikio kikaleta jina la Unanionaje,” amesema Young Killer.

Ameongeza kuwa wimbo huo alitakiwa awepo msanii mwingine wa kike lakini alikosekana. Kwa upande wake Harmonize amesema kuwa anamchukulia Young Killer kama kaka yake kwenye industry na ndiye alimshauri watoe wimbo wa pamoja, na moja kwa moja alikubaliana na wazo lake.

Pia ameongeza kuwa video ya wimbo huo ililipiwa na uongozi wa Wasafi, na waliridhia video hiyo ikafanyike nchini Afrika Kusini.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top