Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Shumileta

MWIGIZAJI wa kitambo Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ au ‘Shumi’ anadaiwa kuwa na hali tete ya kimaisha nchini India kufuatia kile kilichotajwa kuachana na bwana’ke aliyekuwa akiishi naye, raia wa Nigeriahivyo kwa sasa anatafuta msaada wa kurejea nyumbani, Tanzania.

Akizungumza na Wikienda, mmoja wa marafiki wa karibu na Shumileta ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo alisema kuwa, alipata taarifa za masaibu hayo ya Shumileta kutoka kwa mmoja wa wanafamilia yake na kwamba wako kwenye mipango ya kumsaidia arejee nyumbani kuendelea na maisha.

“Ndugu wako kwenye hatua za mwisho kuhakikisha wanamsaidia kurudi nyumbani,” alisema ‘kikulacho’ huyo.

Wikienda liko kwenye msako mkali wa kuwatafuta ndugu wa msanii huyo ili kujiridhisha juu ya madai hayo kuhusu ndugu yao na kila kitu kikikamilika, tutarejea hapa kukujuza kuhusu hali ya Shumi.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top