Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


DIVA anayechipukia kwenye tasnia ya  muziki wa Bongo Fleva,  Haitham Kim,  anayetamba na kibao chake cha Playboy alichomshirikisha nyota wa filamu Bongo,  Wema Sepetu, amesema kuwa wasanii wa kiume wa Bongo ni miyeyusho.

Haitham ambaye yuko chini ya menejimenti ya MJ Records kama msanii rasmi wa rekodi lebo hiyo, amefungukia safari yake ya kimuziki ambapo kidole cha lawama amewanyooshea wasanii wa kiume waliowahi kumnyima ushirikiano na msaada kwa sababu aliwanyima penzi.

Hali hiyo ilisababisha achelewe kutoka kimuziki mpaka siku aliyokutana na prodyuza Daxo Chali ambaye alimpeleka MJ records na akafanikiwa kurekodi ngoma yake ya kwanza inayoitwa fulani na sasa ni Playboy.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top