Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Ikiwa ni takriban miezi minne imepita sasa tangu mkali wa Hiphop nchini Fid Q ata ngaze rasmi kumsaini msanii Big Jahman katika lebo yake ya Cheusi Dawa na kudropisha kitaani ngoma ya Mabundi lakini hadi sasa tumeona ni ukimya ndio ambao umetawala baina ya wawili hao.
Hatuzioni zile mbishe ambazo tumezizoea kuziona kwa mameneja wengine katika kuhangaika kumtafutia matobo msanii kama shows na vitu ka hizo.
kimesogezwa hadi kwa Fareed Kubanda na amebonga na sisi vile ambavyo yeye anaamini meneja anatakiwa kuwa, tofauti na ambavyo wengine wanaamini hadi kufikia hatua ya kumkosoa kuwa huenda yeye sio meneja bora.
“Unajua wengi wanakosea katika maana halisi ya management, management sio kumlipia mtu video au kumlipia mtu studio akarecord audio na kisha kusambaza kwa ma-Djs, management ni kumchukua msanii wako kama product na wewe kuwa na vision ya jinsi ambavyo unaisogeza hiyo product kwenye soko au kwenye jamii kwa ujumla.” Alisema Fid Q.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top