Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Muandaaji wa nyimbo za bongo fleva nchini, Emma The Boy amewataka ma-producer kuacha njaa ili waweze kupata heshima kama anavyopata 'producer' mkongwe Master J.
Emma amebainisha hayo baada ya kuwepo madai ya wasanii wa bongo fleva kutokuwa na nidhamu kwa watarishaji wao wa muziki kwa kile wanachosema kuwa msanii akishatengenezewa 'hit song' huwa hawakumbuki tena mtayarishaji wake wala hata kumpa sifa zake pindi awapo katika mahojiano na vyombo vya habari.
"Ma-producer sisi wenyewe tuna tabia ya njaa, njaa zimezidi. Msanii anakuja na Laki moja au elfu sabini au elfu hamsini kwa sababu ya njaa zako unatengeneza kitu kwa msanii ambaye hana uwezo wa kufanya hivyo. Kwa hiyo mbeleni lazima ikushushe kwa sababu msanii hakuimba kwenye kiwango chake kwa hiyo inakushusha wewe hata kama ulikuwa na ukubwa gani unakosa hiyo heshima", amesema Emma the boy. 
Kwa upande mwingine, Emma amewakumbusha wasanii watambue kuwa ma-producer ndiyo kila kila kitu kwa wasanii kwani nyimbo yako ikiwa mbaya haitaweza kufika kokote pale.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top