Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amedai muziki wa rapa Nay wa Mitego hautofautiani sana na muziki wa Gigy Money na Amber Lulu huku akidai ni muziki uliotawaliwa na majungu na majigambo.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Dudu amewashangaa mashabiki wa muziki kuendelea kumpatia support rapa huyo wakati haoni chochote anachofanya kwenye muziki.
“Mimi sio shabiki wa muziki wa Nay wa Mitego, kwanza muziki wake haueleweki ndio maana namfananisha na Amber Lulu na Gigy Money,” alisema Dudu Baya. “Kuna wasanii wakali wanafanya muziki mzuri kuliko huyo lakini hawapewi support, mimi ningewashauri tu mashabiki wa muziki wapende muziki mzuri,”
Alisema hajui rapa huyo anafanya muziki wa namna gani kwani amekuwa ni msanii wa hip hop anayetumia mwamvuli wa hip hip kuwasema watu.
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki kusikiliza muziki mzuri ambao utawajenga na sio muziki ambao ndani yake una maneno ya kuwasema watu bila sababu.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top