Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Msanii wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol amesema hadi msanii kufanikiwa katika ngazi ya kimataifa si lazima kufanya kazi na msanii mkubwa wa nje.

Hitmaker huyo wa wimbo ‘Phone’, amedai msanii kutengeneza muziki mzuri pekee kunaweza kumfikisha mbali bila kutengemea kubebwa katika kolabo.

“Kwanza wakati mwingine ni sound yako ulivyoifanya kwa mahudhui ya muziki wako, kwa sababu sisi tumewajua wakina Roberto na Amarula imepenya Afrika nzima akiwa pekee yake hata hajaimba na msanii wa Tanzania au hata wa East Afrika,” Ben Pol ameiambia Dj Show ya Radio One na kuongeza.

“Kwa hiyo wakati mwingine ni vibe tu na midundo yako unavyopiga na vile vionjo unavyoviweka. Kuna vionjo vingine hata mtu wa Vietnam au Singapore anaweza kuvibe nayo,” amesistiza Ben Pol.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top