Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Dereva na utingo wa basi la kampuni ya Bunda Express linalofanya safari zake Mwanza- Shinyanga wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Mirungi kiasi cha bunda 112
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna DCP Ahmed Msangi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Sudi Yusuph (35) mkazi wa Buzuruga mkoani Mwanza na Boniphace Mashauri (52) mkazi wa Musoma, Mara
Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba basi hilo linajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya ndipo askari waliweka mtego na kufanikiwa kulikamata katika kijiji cha Misungwi na kuanza upekuzi na kukutwa likiwa limebeba mirungi waliyokuwa wamehifadhi ndani ya begi kisha kuweka kwenye buti ya gari hilo.
Kamanda Msangi amesema mtuhumiwa mmoja ambaye pia ni utingo gari hilo ametoroka lakini juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Pamoja na hayo, DCP Msangi amesema wapo katika upelelezi na mahojiano na watuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani. 


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top