Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Producer wa muziki bongo Abydad amedai kudhulumiwa wimbo aliokuwa amemuandalia msanii wake kisha kupatiwa msanii Ommy Dimpoz ambaye  siku ya jana ameuachia rasmi  ulichukuliwa na mtayarishaji Lolli Pop (GoodLuck Gozbert) kwa ajili ya kuuboresha.
Akizungumza  Abydad amesema kwamba ameshtushwa sana kuusikia wimbo mpya wa Ommy Dimpoz kwani yeye na msanii wake walikuwa katika hatua za mwisho za kufanya video baada ya Loly Pop kuanza kumpiga kalenda kurudisha wimbo aliodai anaenda kuufanyia maboresho.
"Hii ni project yangu ambayo niliifanya na msanii wangu mchanga anayeitwa Modala tangu Januari mwaka jana. Wakati naiandaa Lolli Pop alikuwa studio na yeye alishauri kwamba tumsaidie mdogo wetu atoke, kwa hiyo huu wimbo tuuboreshe vitu na kwa vile sisi tuna tabia ya kushirikiana sikuona shida kumpatia kwa kuwa nilimuamini sasa nilikuja kushtuka baada ya jana kuusikia Ommy anautambulisha alafu anasema kaandikiwa na Lolli Pop" Abydad alifunguka.
Mwanamuziki na Mtayarishaji wa muziki Lolli Pop (Goodluck Gozbert)
Pamoja na hayo Abydad amesema kwamba hataweza kuchukua hatua zozote kwa ajili ya kitendo hicho bali amewaaonya watu wote wenye tabia za aina hiyo waweze kuziacha kwani kunaua vipaji vya vijana wenye ndoto za kufikia mafanikio kama waliyonayo wao.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top