Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


        Muigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mume wake Moze Iyobo. MUIGIZAJI wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema alilazimika kusafiri hadi nchini Thailand kufuata dawa ya kupunguza unene baada ya kuona hali hiyo inamnyima raha kwani ingeweza kumfanya aonekane mzee. Akizungumza na Za Motomoto News, Aunt alisema alijitahidi sana kupunguza mwili wake lakini ikawa ngumu ndipo alipoamua kufunga safari hadi Thailand baada ya kuambiwa kuwa kuna dawa ya kupunguza mwili na baada ya kutumia, anaona mabadiliko. 
Dah, yaani hata nikivaa nguo najiona wazi sipendezi hivyo katika pitapita yangu nikaambiwa kuna dawa nzuri Thailand, nikaenda na baada ya kuanza kutumia, naona ina manufaa makubwa na nadhani inaweza kuwasaidia watu wengine wasiopenda unene,” alisema.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top