Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Upo usemi maarufu wa Waswahili unasema ‘Rafiki wa adui yako, ni rafiki yako’ ndiyo inavyoelekea kuwa kwa mahasimu wa kisiasa ambapo baada ya kufanya mazungumzo kwa saa mbili unusu Rais Donald Trump na Rais Vladimir Putin walijumuka pamoja kwa ajili ya chakula cha usiku.
Gumzo halikuwa kwa Trump ambaye alikutana na Putin kwa mara ya kwanza Ijumaa kwenye mkutano wa G20 uliofanyika Hamburg, Ujerumani bali ilikuwa wakati wa chakula cha usiku ambapo Rais Putin alikuwa ubavuni mwa mke wa Trump, Melania Trump.Wakati wote Melania Trump alionekana kuwa karibu na Putin huku Trump akikaa mbali karibu na Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa China Xi Jinping.
Melania Trump amekulia Slovenia, zamani sehemu ya Yugoslavia, na anazifahamu lugha kadhaa ikiwemo Kijerumani ambacho Rais wa Urusi pia huzungumza.

Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top