Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Wapiganaji wa Al Shabab wenye asilia ya kisomali wamewachinja wakenya 9 katika kijiji cha Poromoko siku ya Jumamosi.Kwa mujibu wa habari,polisi wameviambia vyombo vya habari kuwa washambuliaji hao wanahisiwa kuwa wameingia Kenya kupitia mpaka wa Kenya na Somalia.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa nchi yake imepata majanga mawili kwa wakati mmoja kwani Kenya bado ilikuwa inaomboleza kifo cha waziri Joseph Nkaissery.
Vilevile rais Kenyatta amewaahidi wananchi kuwa nchi yake itaongeza mbinu za kulinda usalama wa raia wake.
Hata hivyo polisi wameongezwa kulinda zaidi mahala tokeo hilo lilipotokea.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top