Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Siku mbili tu zimepita tangu mwimbaji wa Bongofleva Ommy Dimpoz kuutambulisha wimbo wake mpya ‘Cheche’ lakini leo July 8, 2017 ameibuka Producer Abydaddyakichukua headlines kwenye mitandao akilalamika kuwa Ommy Dimpoz amechukua chorus yake na kuitumia bila ridhaa yake.
Abydaddy ”Kikubwa ambacho naweza kukiongelea ni kwamba, huo wimbo ni mali yangu…namaanisha kwamba, kuna wimbo nilikuwa naanda ulikuwa unaitwa Cheche na siku nikiandaa huo wimbo studio kwangu nilitembelewa na producer Lolipop na aliniambia ameipenda basi nikamruhusu aichukue.
Lengo la mimi kumkabidhi ni kwamba aimalizie kisha amkabidhi msanii wangu aitwae Modala kwani ndio makubaliano yenu lakini sio wazo la chorus na mdundo visikike kwa Ommy Dimpoz” – Abydaddy.


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top