Pages

Labels

Friday, September 14, 2012

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA MJINI MAGU Shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mbogamboga la Ngongoseke lililoko katika kijiji cha Nsola wilayani Magu ni mfano wa kuigwa katika  matumizi ya ziwa Victoria. Pichani, nyanya ndogondogo maarufu kwa jina la nyanyapori zikiwa zimelimwa kitalaam kwenye shamba hilo ambalo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilitembelea Septemba 13, 2012.
 Mtoto akiwa  amenyanyuliwa juu ili aweze kumwona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa Sabasaba Mjini Magu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza, Septemba 13, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua gati la kupokelea samaki katika kijiji cha Kigangama wilayani Magu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza, Septemba 13, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

UNICEF YALIPIGA JEKI JESHI LA MAGEREZA VIFAA VYA USD 8,972


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Pereira Silima (kulia) akipokea msaada wa kijamii kutoka kwa Mwakilishi Msaidizi wa kitengo cha  kuunganisha watoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa ( UNICEF) nchini  Paul Edwards (kushoto) leo jijini Dare es Salaam. Msaada huo una vitu mbalimbali kama vyandarua, magodoro, mito, taulo  na vifaa vya michezo.venye thamani ya dola za kimarekani 8,972. Kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Fidelis Mboya,
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Pereira Silima, akizungumza machache baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Magereza waliohudhuria Hafla ya makabidhiano ya msaada  wa kijamii wa  Vifaa mbalimbali  kutoka UNICEF kwa watoto waliopo Magereza mawili ya watoto nchini Segerea na Ruanda (Mbeya), Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Slaam. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS, ZANZIBAR, MHESHIMIWA MAALIM SEIF HAMMAD KUKUTANA NA WATANZANIA LEO JIONI NCHINI UINGEREZA


 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad, siku ya Alhamisi tarehe 14/9/12 alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuria na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe
 Makamu wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Bwana  David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi linalotolewa na BTS,  Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-  Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akiwa pamoja na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Seif alikutana na Mabalozi hao jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. Katikati ya picha ni Mheshimiwa, Makamu wa Rais, Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kushoto), Balozi wa Rwanda, Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (Pili kushoto), Balozi wa Uganda, Mheshimiwa Joan Rwabyomere (Pili kulia), na Balozi Mdogo wa Burundi, Mheshimiwa Bernard Ntahiraja (Kwanza kulia).
--
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, aliendelea na Ziara yake ya jana hapa nchini Uingereza. Mheshimwa Seif, jana alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais, aliweza kukutana na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki na Viongozi wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi Tanzania, ijulikanayo kama Britain Tanzania Society (BTS).

Leo hii siku ya Ijumaa, Jioni, kuanzia Saa 18:00pm mpaka saa 21:00, Mheshimiwa Makamu wa Rais atakutana na Watanzania wote waishio London, katika Ukumbi wa University of London Union, Mtaa wa Malet Street, WC1E 7HY

Watanzania wote wenye nafasi ya kufika mnakaribishwa.

Watakao hudhuria mnaombwa sana kuzingatia muda uliopangwa.

Taswira mbalimbali za Ziara rasmi ya Rais Jakaya Kikwete Nchini Kenya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais jakaya kikwete akiweka shada la maua kwenye kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Mama Salma Kikwete akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi. Kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho
Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho
Rais Kikwete akiangalia ng'ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n6- Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n7- Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja n ujumbe wake na wanachuo na viongozi wa chuo hicho baada ya kukitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, Picha na IKULU

MKUTANO WA UANZISHWAJI WA ENEO HURU LA MAGONJWA YA MIFUGO KATIKA MKOA WA RUKWAPicha ya pamoja kati ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang’a na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Winston Mleche pamoja na wataalamu wa Mifugo kutoka Mikoa ya Rukwa, Njombe, Katavi, Tabora, Mbeya, Singida, Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Iringa, Kagera, Mara, Simiyu na Geita katika kikao kilichowashirikisha wataalamu hao katika kujadili mpango wa kuanzishwa eneo huru la magonjwa ya mifugo katika Wilaya za Sumbawanga na Nkasi Mkoani Rukwa kwa lengo la kuwezesha kufanyika kwa biashara ya mifugo na mazao ya mifugo kwa kufuata vigezo na masharti ya kimataifa.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwakaribisha wageni hao Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya mifugo mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Moshi Chang’a ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya ambaye yupo safarini kikazi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Winston Mleche ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za mifugo nchini. Katika hotuba yake hiyo alielezea changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ikiwemo uimarishaji wa mifumo ya usafirishaji, uchukuzi na mawasiliano, kuboresha miundombinu ya masoko ya mifugo, kuendelea kuboresha aina ya mifugo na mifumo ya uzalishaji mifugo, kuboresha taratibu za umiliki wa ardhi na kuzuia magonjwa mbalimbali ya mifugo. Hata hivo Mkoa wa Rukwa umepiga hatua kubwa katika kupambana na magonjwa hatarishi ya mifugo ambayo kwa sasa yapo kwa kiwango kidogo sana.
Daktari wa Mifugo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Loomu akiwasilisha mada ya fursa za mifugo zinazopatikana Mkoani Rukwa. Zipo fursa nyingi Mkoani Rukwa ikiwemo mifugo mingi na ya aina tofauti yenye afya pamoja na wafugaji mahiri wadogo na wakubwa. ,Maeneo ya malisho, uwepo wa kiwanda cha kisasa cha nyama cha Saafi kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndaji ni fursa nyingine.

Matukio Mbalimbali Katika Ziara JK Nchini Kenya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akitembelea Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipanda miti wakati walipozuru mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke utokao chini ya ardhi wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini Kenya.

Mwandishi Afukuzwa Uanachama Baada Ya Kuwasaliti WenzakeMUSOMA

CHAMA cha Waandishi wa Habari mkoani Mara MRPC, kimemfukuza uanachama wa chama hicho, mwandishi wa habari wa radio Free Afrika mkoani Mara Bw Maxmilian Ngesi baada ya kukiuka makubalino ya chama hicho yaliyofikiwa juzi ya kutoandika kabisa habari za jeshi la polisi mkoani humo.

Akizungumzia kufukuzwa kwa Mwandishi huyo mwenyekiti wa chama hicho Bw Emmanuel Bwimbo,alisema kuwa Ngesi amekiuka makubaliano ya waandishi wenzake na chama kwa ujumla baada ya kusikika akitangaza habari za jeshi la polisi kwa kumkariri kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara.

“ Sisi kwa kauli moja tumekubaliana kutofanya kazi na Jeshi la Polisi Mkoani Mara baada ya Matukio kadhaa likiwemo ya kuuawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa na kutunyima kibali cha Maandamano yetu ya Amani kupinga Mauaji hayo” alisema Bw Bwimbo

Bw Bwimbo alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani mwandishi huyo alivyokiuka makubaliano ya pamoja na kuwasaliti wenzake ambao wamekubaliana kwa pamoja kuwa hawataandika habari za jeshi hilo kutokana na kuzuiwa waandishi kutoandamana katika maandamano ambayo yaliitishwa nchini kote kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa kituo cha chanel Ten mkoani Iringa Daud Mwangosi.

Alisema Ngesi kama mwanachama alitakiwa kutii maamuzi ya chama na tamko la chama chake kwa vile tamko hilo limewataka wananchama wote na siyo kwa mkoa wa Mara tu lakini pia baadhi ya mikoa imetoa matamko na misimamo hiyo lakini cha kushangaza yeye amekaidi na kwenda kinyume.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia mwandishi atakaye kiuka agizo hilo na hatua ambayo imechukuliwa kwa Ngesi ni mfano kwa waandishi wengine hadi hapo tamko hilo litakapo tenguliwa.

Jumatatu wiki hii waandishi wa habari walifanya maandamano nchi nzima wakilaani mauaji ya mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi ambapo kwa mkoa wa Mara maandamano hayo yaliuzuiwa na polisi hali iliyofanya chama cha waandishi wa habari kukataa kuandika habari za jeshi hilo mkoani Mara.

POLISI WATANDA MITAANI KUZUIA NJAMA ZA KUMUONDOA MADARAKANI MUFT MKUU WA TANZANIADar es Salaam yetu tumetegesha kamera zetu maeneo yote na kwa lolote litakalojitokeza tutakuletea taarifa

Taswira Za Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ambae pia ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika Dk. Terezya Huvisa akiongoza kikao cha mawaziri hao katika ukumbi wa AICC mjini Arusha leo.
Baadhi ya Mawaziri wa Mazingira barani Afrika wakimsikiliza Rais wa Mawaziri wa Mazingira Afrika Dk. Terezya Huvisa (hayupo pichani) katika mkutano unaoendelea mjini Arusha kwenye ukumbi wa AICC.Picha na Ali Meja

KUTOKA DODOMA:Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM)Wamaliza kikao cha baraza; Yainyooshea kidole CHADEMA kwa matukio ya mauajiUkumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Taifa UVCCM,ambae pia ni mjumbe kikao Cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Ridhwan J. Kikwete akichangia hoja katika kikao Cha Baraza hilo kilichofanyika jana, tarehe 12, Makao Makuu ya Chama,Dodoma
Kutoka kulia Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Ndugu Martine Shigela akichangia ajenda katika kikao cha Baraza la Umoja huo,(katikati) ni Makamu Mwenyekiti Ndugu Beno Malisa na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mfaume kizigo, wakiwa katika kikao cha Baraza hilo kililofanyika Jana tarehe 12 katika ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
Mjumbe wa UVCCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdalah Ulega
Mmoja wa wajumbe wa Baraza ambae pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Dar es salaam, Ndugu Said Mtimizi akiwa katika Kikao hicho cha Baraza kilichofanyika jana, Sept 12, Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la UmojawaVijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakifuatilia hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wa kupitisha majina ya wagombea wanafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa na Taifa.

Baadhi ya maafisa na watendaji waUmoja waVijana,Wa kwanza kushotoNdugu Shara Ahmed (Mkuu wa Kitengo Cha Oganaizesheni Unguja) Ndugu John Milele (Mkuuwa Kitengo cha Fedha na Uchumi) Ndugu Deogratius Daffi (Mhasibu Mkuu) na Ndugu Salmin Dauda(mwenye laptop) Mkuu wa Kitengo Cha BenkiyaVijana)

Wajumbe wa Baraza la Vijana Kutoka Tanzania, Zanzibar ambao pia ni wajumbe wa halmashauri kuu ya Chama Taifa (NEC) wakiwakilisha vijana kutoka Zanzibar, Ndugu Hawa Sukwa na Ndugu Hadillah Vuai (mwenye Chupa ya maji).

Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakifuatilia hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wakupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa na Taifa.

Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Barza la UVCCM, kutoka kulia, safu ya mbele Salmin Dauda (Mkuu wa kitengo cha Benki ya Vijana), Tumaini Mwakasege (Katibu Msaidizi Siasa na Oganaizesheni, Vyuo Vikuu) na Abdallah (Mkuu wa Utawala Ofisi ndogo UVCCM, Zanzibar)
---
Na Suleyman Mwenda,
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wamemaliza kikao cha baraza la umoja huo ambapo wamejadili ajenda mbalimbali za msingi kuhusu Uchaguzi na pia wamejadili juu ya hali ya siasa nchini na mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji, ambapo wamekinyooshea kidole Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwa vinara wa matukio ya mauaji, kitu ambacho ni hatari kwa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya Katibu Mkuu, jengo la Mikutano (whitehouse) katika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi, Dodoma.
Alisema kuwa, kumekuwa na matukio ya mauaji kwenye mikutano ya chama hicho katika mikoa ya Singida, Igunga, Tabora, Morogoro na Iringa hali ambayo imekuwa ikitishia Usalama na Amani ya Nchi.

“Tunalaani Chadema kuwa vinara wa vurugu zinazosababisha mauaji na kila tukio linapotokea viongozi wa Chadema wanakuwepo, hali inayoonyesha kuwa siasa wanazoendesha si za kistaarabu” alisema.

Alisema kuwa Chadema wanachojenga ni hatari kwa Taifa na pia hatari kwa Umoja wa Vijana pia na kama wana mapenzi ya kweli na watanzania waache siasa zinazasababisha mauaji mara kwa mara.

Katika hatua nyingine, Shigela amesema kuwa,Kikao cha baraza Kuu kilimalizika jana na kufanya maamuzi baada ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea na baadhi ya nafasi majina yatapelekwa halmashauri kuu ya taifa (NEC) ambacho ni chombo cha mwisho cha maamuzi katika Chama.

Amezitaja nafasi ambazo tayari zimetolewa maamuzi, kuwa ni nafasi ya mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda UWT, Mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda wazazi, Baraza Kuu taifa nafasi tano Zanzibar na nafasi tano Bara, na sasa orodha hiyo inaandaliwa ili majina ya waliochaguliwa yatangazwe rasmi.

Amesema kuwa,katika nafasi nyingine ikiwemo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti tayari yamewekewa alama na yatapelekwa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC).

Pia amewataka wagombea ambao tayari wamefanyiwa uteuzi waache siasa za kuchafuana na zile za makundi.

Aidha alisema kuwa Mkutano Mkuu wa taifa unatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 20, mwaka huu na kutaka wajumbe wote kuhakikisha wanafika Dodoma Oktoba 19.

Shigela amesema kuwa, Baraza kuu lilipata nafasi ya kuwapongeza vijana wa Jumuiya kwa kuthibitisha kuwa umoja huo ni tanuru la kuoka viongozi kwa baadhi yao kuteuliwa nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Chama na kulitaka Baraza kuu kuzingatia mahitaji ya vijana ili wapate fursa zaidi za kugombea ili umoja huo uweze kupeleka sura nyingi za vijana ndani ya chama.

Pia alisema kuwa wametapa nafasi ya kuitafakari taarifa ya kazi nzuri ya Serikali kwa kuwawezesha vijana katika suala la kuwapatia elimu na kuwawekea mikakati ya miaka mitano ya kusaidia vijana.

Shigela aliitaka Serikali kuwa na mipango ya kudumu ili kuweza kudhibiti majanga mbalimbali yanayotokea hapa nchini k.v mafuriko, kuzama kwa meli, mauaji n.k.

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari- Ligi Kuu Ya Vodacom Tanzania Bara Kuanza Kesho                              Release No. 145
             TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                        Septemba 14, 2012

VPL 2012/2013 KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara 2012/2013 inaanza kutimua vumbi kesho (Septemba 15 mwaka huu) ambapo timu zote 14 zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti.

Mabingwa watetezi Simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mjini Morogoro, Polisi Dodoma watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati jijini Tanga, Mgambo JKT ambayo imepanda daraja msimu huu itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Tanzania Prisons ambayo nayo imerejea VPL msimu huu itaialika Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. JKT Ruvu na Ruvu Shooting zitapambana kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam huku Azam ikiwatembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto Africans dhidi ya Oljoro JKT. Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.

Viingilio katika mechi ya Simba na African Lyon vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Viingilio kwa mechi nyingine vitakuwa sh. 3,000 na sh. 10,000.

                                   Boniface Wambura
                                        Ofisa Habari
                   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

BWENI LATEKETEA KWA MOTO NJOMBE, WANAFUNZI 93 WANUSURIKA KIFO


WANAFUNZI 93 wamenusurika kufa baada ya bweni lao kutekea kwa moto usiku wa kuamkia leo katika shule ya sekondari ya wasichana ya Wanike iliyopo Kata ya Mdandu wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe.

Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Estelina Kilasi amesema, tukio hilo limetokea septemba 13 saa 4 usiku na kuteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi hao ambavyo thamani yake bado haijajulikana na chanzo cha moto huo hakijafahamika.aa

Bi Kilasi amsema, bweni ambalo limeteketea ni la wasichana wanaosoma kidato cha tatu na cha nne ambao wote walifanikiwa kutoka nje na kuacha mali zao zikiteketea kwa moto.

Amevitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja ni daftari, vitanda, magodoro na nguo za kiraia na sare zao vyote vimeteketea kwa moto huo.

Kutokana na ajali hiyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza wazazi wote kufika shuleni hapo septemba 16 ili kujadili kwa pamoja kuhusiana na tatizo hilo.
Blogzamikoa

NMB YAWAZAWADIA WASHINDI WA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB


Kaimu meneja Tawi la NMB Mbalizi road John Chinguku akimkabidhi tani moja ya mifuko sementi mshindi wa promosheni ya jenga maisha yako na NMB Bi Akson Sheyo Mwinga huku Meneja NMB kanda ya nyanda za juu Lucresia Makiriye pamoja na watumishi wengine wakishuhudia tukio hilo la utoaji zawahi hizo


Baadhi ya washindi wa promosheni ya jenga maisha yako na NMB wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao


Jenga Maisha Yako na NMB ni promosheni iliyoanzishwa na NMB baada ya kugundua kuwa watanzania wengi wana matarajio na malengo wanayotaka kuyatimiza maishani, kama vile; kumiliki nyumba nzuri, kusomesha watoto shule nzuri na mambo mengine mazuri.
NMB inapenda kuwasaidia watanzania wote ili kuhakikisha wanafikia ndoto zao katika maisha waliojipangia, hivyo basi ndipo NMB ikaja na msingi wa kuzifikia ndoto hizo unaojulikana kwa jina la Jenga Maisha Yako na NMB.

Jenga Maisha Yako na NMB ni promosheni iliyounganishwa na akaunti za NMB Junior akaunti na NMB Bonus akaunti. Promosheni hii itawaingiza moja kwa moja wateja waliofungua NMB Bonus akaunti au NMB Junior akaunti wenye kiwango kisichopungua shilingi 50,000 au kinachozidi hapo ili kushinda zawadi mbalimbali.

HUYU ndo KIJANA anaye dai JUMA NATURE ni BABA YAKE ILA AMEMKATAA

kijana huyu anaeitwa Samson, ameibuka  na kudai Juma Nature ni baba yake ila amemkataa

Taswira Mbalimbali Za Mkutano wa Kampeni wa Chama cha TADEA Zanzibar

Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha TEDEA Seif Salim Seif, akitowa sera za Chama chake katika mkutano wake wa kampeni katika viwanja  vya mpira Chagua Kijichi Bububu.
Katibu Mkuu wa Chama cha TADEA Ali Juma Ali akimnadi Mgombea wa Chama chake katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu Seif Salim Seif katika mkutano wao wa kampeni katika kiwanja cha ChaguaKijichi Bububu.
 Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha TEDEA Seif Salim Seif, akitowa sera za Chama chake katika mkutano wake wa kampeni katika viwanja  vya mpira Chagua Kijichi Bububu.
 Katibu Mkuu wa Chama cha TADEA Ali Juma Ali akimnadi Mgombea wa Chama chake katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu Seif Salim Seif katika mkutano wao wa kampeni katika kiwanja cha Chagua
Viongozi wa Chama cha  TADEA, wakimsikiliza Mgomea wao katika mkutano wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu wakati wa mkutano wao wa kampeni katika viwanja vya Chagua Kijichi..
 
 
Blogger Templates