Featured
Loading...

AZAM NA SIMBA NANI MKALI LEO ZANZIBAR


Kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall,
ataendelea kuwa simu ya vigogo wa soka Tanzania?


MICHUANO ya Kombe la Urafiki, inayondaliwa na Chama cha Soka Zanzibar, inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mkali na wa kusisimua kati ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC na Azam FC kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo wa Kundi A unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na ukweli kwamba Azam ndio washindi wa pili wa Ligi Kuu.
Aidha, mechi baina ya timu hizo siku za karibuni zimekuwa zenye upinzani mkali na ikizingatiwa timu zote zitashiriki Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame- basi kila upande utataka kuwatia moyo mashabiki wake.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ‘Mr. Liverpool’ alisema jana kwamba wana matumaini ya kuifunga Azam FC leo, ili wawadhihirishie wao ndio ‘Baba ya soka Tanzania’.
Kwa upande wake, Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa alisema nao wako vizuri na wamejipanga vema kuifunga Simba SC.
Katika mechi yake ya kwanza juzi, Simba SC ilianza vyema baada ya kuifunga Mafunzo mabao 2-1, wakati Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na U23, Karume Boys.
Mabao yote ya Wekundu wa Msimbazi yalitupiwa nyavuni na mshambuliaji mpya, aliyesajiliwa kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, Abdallah Juma, ambaye amepokewa Simba kama Emmanuel Gabriel mpya. Dullah alifunga mabao hayo dakika ya 27 na 44, yote akiunganisha pasi za kuingo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Patrick Kanu Mbivayanga, wakati Mafunzo walipata bao lao kufutia machozi dakika ya 80, mfungaji Jaku Joma.
Azam wao juzi walilazimika kusubiri hadi dakika ya 79 kupata sare ya 1-1 kwa bao la mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Tcheche, baada ya Karume Boys kupata bao la kuongoza dakika ya 45 kwa njia ya penalti, mfungaji Ibrahim Hamisi.
Katika mechi za kwanza za Kundi A jana, Yanga ya Dar es Salaam pia, ilifungwa kwa taabu mabao 3-2 na Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Yanga ambayo imepeleka wachezaji wake wa kikosi cha vijana visiwani humo, hadi mapumziko, ilikuwa tayari nyuma kwa mabao 2-1.
Lakini kipindi cha pili, Yanga B walikuja juu na kucheza soka ya kuvutia, ingawa waliishia kukosa mabao ya wazi kabla ya kupata moja na wapinzani wao wakipata moja zaidi pia .
Kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkock,
ataendelea kucheka leo>
 SOURCE BIN ZUBERY
Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 – 14 October 1999) was a Tanzanian statesman who served as the leader of Tanzania, and previously Tanganyika, from 1960 until his retirement in 1985.[2] Born in Tanganyika to Nyerere Burito (1860–1942), Chief of the Zanaki,[3] Nyerere was known by the Swahilihonorific Mwalimu or 'teacher', his profession prior to politics.[4] He was also referred to as Baba wa Taifa (Father of the Nation).[5] Nyerere received his higher education at Makerere University in Kampala and the University of Edinburgh. After he returned to Tanganyika, he worked as a teacher. In 1954, he helped form the Tanganyika African National Union.. Check her out:
Newer Posts Older Posts
© Copyright MATUKIO NA VIJANA | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top