Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail ThisHatimaye klabu ya Orlando Pirates imetuma rasmi barua ya mualiko kwa mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuweza kujiunga na timu hiyo.
Hii ni sehemu ya barua ya Orlando kumualika Okwi.
Nimefanikiwa kuiona barua hiyo ikiwa inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akihudumiwa kuanzia usafiri, malazi, matibabu pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza kwa wakati atakaokuwa na klabu hiyo.

Kwa kipindi cha misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi ambaye klabu yake ya Simba imemuwekea price tag ya Billioni 2 kwa timu inayomtaka, huku pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga ikiwa inamfukuzia mshambuliaji huyo wa Uganda ambaye siku za hivi karibuni amekuwa ndio tegemeo la safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa Tanzania.kwa hisani ya shaffih dauda


Facebook Blogger Plugin by

Post a Comment

 
Top