Featured
Loading...

HATIMA YA MWILI WA MAWAZO KUAGWA AMA KUTOAGWA JIJINI MWANZA KUJULIKANA KESHO.

Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha kesi ya madai ya kuomba ridhaa ya kufanya ibada ya Mazishi ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoani Geita Marehemu Alphonce Mawazo iliyowasilishwa na Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi wa marehemu Mawazo.

Katika kesi hiyo, mlalamikaji anaiomba mahakama kuondoa zuio la jeshi la polisi Mkoani Mwanza la kutoruhusu shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mawazo kufanyika Jijini Mwanza, kabla ya kwenda kuzikwa Mkoani Geita.

John Mallya ambae ni miongoni mwa Mawakili watatu wa Chadema ambao wanaitetea kesi hiyo, amebainisha kuwa Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi kesho majira ya saa saba mchana, ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha anatarajiwa kutoa maamuzi yake baada ya leo kusikiliza utetezi wa pande zote mbili zinazohusika.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema bara Salum Mwalimu, amewasihi wanafamilia pamoja na wafuasi wa chama hicho kuendelea kuwa watulivu, wakati maamuzi ya mahakama hiyo yakisubiriwa ambapo ameeleza kuridhika na mwenendo wa kesi hiyo.

Nje ya Mahakama, ulinzi ulikuwa umeimarishwa zaidi ambapo kulikuwa na polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa na bunduki za risasi za moto, mabomu ya machozi pamoja na mbwa ambapo baada ya kesi hiyo kuahirishwa, umati mkubwa wa wananchi uliokuwa umetanda mita chache kutoka Mahakamani hapo ulianza kuimba nyimbo za maombolezo na kuwasindikiza viongozi mbalimbali wa chedema hadi katika hoteli waliyofikia. 
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA BINAGI RADIO-HABARI 
John Mallya ambae ni mmoja wa Mawakili wa Chadema akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Katibu Mkuu Msaidizi Chadema bara, Salum Mwalimu akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Viongozi na makada wa Chadema wakiwa mahakamani
Viongozi na makada wa Chadema wakiwa mahakamani
Mawakili na Viongozi/Makada wa Chadema wakitoka Mahakamani
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakitoka Mahakamani huku wakiimba nyimbo za maombolezo
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakitoka Mahakamani huku wakiimba nyimbo za maombolezo
Wananchi hawa waliwasindikiza viongozi wa chadema hadi hotelini.

KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI PAPA FRANCIS AWASILI KENYA JIONI HII,

Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na kumpokea Kiongozi wa kanisa la katoliki duniani Papa Francis muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya jioni hii

MAGAZETI YA UDAKU LEO

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 25.11.2015BARCELONA YAITWANGA ROMA 6-1,MESSI SUAREZ MOTO MKALI

Barcelona sasa haishikiki, kama unabisha waulize AS Roma ya Italia.
Baada ya kuitwanga Real Madrid mabao 4-0 katika mechi ya La Liga, leo imeangushia kipigo AS Roma cha mabao 6-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi na Luis Suarez ambao kila mmoja amefunga mawili, Gerard Pique na Adriano kila mmoja akafunga moja
Eden Dzeko alifunga bao pekee la Roma lakini akakosa kufunga mkwaju wa penalti kama ilivyokuwa kwa Neymar.

BAYERN MUNICH YAENDELEZA VIPIGO LIGI YA MABINGWA ULAYA

Bayern Munich bado kiwembe asee! Imeikong’ota Olimpiakos ya Ugiriki kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Sasa ina uhakika wa kila kitu katika hatua ya mtoano na shukurani zinaenda kwa Douglas Costa, Robert Lewandwski, Thomas Muller na Kingsley Coman.

ARSENAL YAICHAPA DINAMO 3-0 LIGI YA MABINGWA ULAYA

Kama ulidhani Arsenal imelala Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi ulijidanganya, maana imeitandika Dinamo Zagreb kwa mabao 3-0.
Ikiwa nyumbani Emirates jijini London, Arsenal imeibuka na ushindi huo wa mabao manne yaliyofungwa na Mesut Ozil, Alexis Sanchez aliyefunga mawili.

Arsenal: Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini, Cazorla, Campbell, Ozil, Sanchez, Giroud.
Subs: Ospina, Debuchy, Gibbs, Gabriel, Ramsey, Chambers, Reine Adelaide.
Dinamo Zagreb: Eduardo, Ivo Pinto, Sigali, Taravel, Matel, Paulo Machado, Goncalo, Antolic, Pjaca, Rog, Fernandes.
Subs: Mikulic, Soudani, Musa, Sovsic, Henriquez, Pavicic, Coric.
Referee: Viktor Kassai (Hungary)


LIGI YA MABINGWA ULAYA,CHELSEA WAICHAPA MACCABI HAIFA

Chelsea imeitwanga Maccabi Haifa kwa mabao 4-0 ikiwa nyumbani Tel Aviv, Israel.
Mabao ya Chelsea katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamefungwa na Cahill, William, Oscar na Zouma.
CHELSEA: Begovic; Azpilicueta, Cahill, Terry (c)/Zouma, Rahman; Fabregas, Matic; Willian, Oscar, Hazard/Pedro; Costa
SUBS: Blackman, Ivanovic, Zouma, Mikel, Loftus-Cheek, Pedro, Remy
Kwa ushindi huo, Chelsea imechukua uongozi wa Kundi G baada ya kufikisha pointi 10, sawa na FC Porto ambayo imechezea kichapo cha mabao 2-0.
Older Posts
© Copyright MATUKIO NA VIJANA | Designed By TOLEOJIPYA.COM
Back To Top